Social Icons

Tuesday, December 23, 2014

UONGOZI SIO KIZIZI NI UWAJIBIKAJI


Simulizi hii, inasimulia habari za mtu aliepewa dhamana ya kuwawakilisha wananchi, lakini akawasahau pindi alipofanikiwa, sasa uchaguzi umefika, anaamini kwamba kizizi na miujiza vitaweza kumpa ushindi pale aliposhindwa kuwajibika kwa kutumikia umma wake, Hebu itazame na utoe maoni yako .

Sunday, December 21, 2014

MGOMBEA WETU KARUDI !!

Simulizi hii inazungumzia jinsi gani badhi ya wagombea , baada ya kuwa wamepata dhamana ya kwenda kuakilisha wananchi, hua wanakaa huko huko na kuwasahau wale waliowapa dhamana, sasa uchaguzi unapokuja wanaanza kukumbuka kuwakaribia wananchi, matokeo yake wanakutana na vijana kama hawa ambao wana uchungu na maendeleo, na kujikuta katika mgogoro nao, hebu tazama na utoe maoni .

MMOMONYOKO WA MAADILI

Simulizi hii inaonyesha changamoto zinazotokana na walimu ambao bado ni vijana wanaopewa kazi za kufundisha, pindi wanapomaliza vyuo, na hivyo kujikuta katika mahusiano na wanafunzi wa kike na wakati mwingine kujifanya vidume kupelekea majanga kama haya. Maadili ya kulea na kufundisha wanafunzi wa sekondari, yanapaswa kuzingatiwa kabla ya kupewa kazi, tusije tukajikuta tuna waalimu wa namna hii, tazama na utoe maoni yako.

Tuesday, December 9, 2014

BON IYAIYA

Ni ukatili wa kijinsia mtupu , lakini sasa basi , toa maoni yako

MIKOPO

VIKUNDI VYA VIJANA NI MOJA WAPO YA WATHIRIKA WAKUTOKUAMINIWA KWA KUPEWA MIKOPO YA KUJIENDELEZA , JE TATIZO NI NINI ?, TAZAMA HII HAPA NA UTOE MAONI YAKO



TAMAA

Kuna wazazi wengine ambao wanafurahishwa na vijizawadi wanavyoletewa na mabinti zao bila kujali vimetoka wapi ? matokeo yake mwisho wanalipa gharama ya zawadi zile kwa uhai wa mabinti zao , je umeshawahi kuyaona haya ? hebu tazama na utoe maoni


NDOA ZA UTOTONI

Wajanja wengi na watu wenye tamaa wanatumia, visingizio vya imani, na tamaduni, kuwarubuni mabinti, na kuwafanya kabisa wapoteze ndoto zao za maisha ya usoni, na kuwafanya wajikute katika ndoa za utotoni, lakini kwa kizazi hiki, jamii iko makini sana, kijana umeumbuka baada ya kujikuta ameshughulikiwa na mzazi wa binti alietaka kurubuni, hebu itazame hii na utoe maoni yako.

MADAWA HOSIPITALINI

mara nyingi watu wakienda hospitalini wanaambiwa kwamba hakuna madawa , lakini wanaelekezwa kwenye maduka fulani , nini ambacho kiko nyuma ya pazia ? tazama hapa ?

ITIKADI TOFAUTI


Changamoto zinazotokana na wanandoa kuwa katika vyama tofauti, umewahi kushuhudia changamoto za namna hii ?, toa maoni yako sasa.

AFYA KUZOROTA

Vifo vya akina mama wajaa wazito vingi vinasababishwa na ukosefu wa huduma  za afya pamoja na wahudumu wa afya kutokuajibika

KAULI ZA VIJANA

Vijana wengi wanashabikia mabadiliko lakini hawajiandikishi na kuchukua vitambulisho vya kupiga kura , sasa mabadiliko wanayoyatarajia, na viongozi waadilifu watapatikana vipi ? Hebu toa maoni yako kuhusiana na jambo hili.