Social Icons

Tuesday, December 23, 2014

UONGOZI SIO KIZIZI NI UWAJIBIKAJI


Simulizi hii, inasimulia habari za mtu aliepewa dhamana ya kuwawakilisha wananchi, lakini akawasahau pindi alipofanikiwa, sasa uchaguzi umefika, anaamini kwamba kizizi na miujiza vitaweza kumpa ushindi pale aliposhindwa kuwajibika kwa kutumikia umma wake, Hebu itazame na utoe maoni yako .

Sunday, December 21, 2014

MGOMBEA WETU KARUDI !!

Simulizi hii inazungumzia jinsi gani badhi ya wagombea , baada ya kuwa wamepata dhamana ya kwenda kuakilisha wananchi, hua wanakaa huko huko na kuwasahau wale waliowapa dhamana, sasa uchaguzi unapokuja wanaanza kukumbuka kuwakaribia wananchi, matokeo yake wanakutana na vijana kama hawa ambao wana uchungu na maendeleo, na kujikuta katika mgogoro nao, hebu tazama na utoe maoni .

MMOMONYOKO WA MAADILI

Simulizi hii inaonyesha changamoto zinazotokana na walimu ambao bado ni vijana wanaopewa kazi za kufundisha, pindi wanapomaliza vyuo, na hivyo kujikuta katika mahusiano na wanafunzi wa kike na wakati mwingine kujifanya vidume kupelekea majanga kama haya. Maadili ya kulea na kufundisha wanafunzi wa sekondari, yanapaswa kuzingatiwa kabla ya kupewa kazi, tusije tukajikuta tuna waalimu wa namna hii, tazama na utoe maoni yako.

Tuesday, December 9, 2014

BON IYAIYA

Ni ukatili wa kijinsia mtupu , lakini sasa basi , toa maoni yako

MIKOPO

VIKUNDI VYA VIJANA NI MOJA WAPO YA WATHIRIKA WAKUTOKUAMINIWA KWA KUPEWA MIKOPO YA KUJIENDELEZA , JE TATIZO NI NINI ?, TAZAMA HII HAPA NA UTOE MAONI YAKO



TAMAA

Kuna wazazi wengine ambao wanafurahishwa na vijizawadi wanavyoletewa na mabinti zao bila kujali vimetoka wapi ? matokeo yake mwisho wanalipa gharama ya zawadi zile kwa uhai wa mabinti zao , je umeshawahi kuyaona haya ? hebu tazama na utoe maoni


NDOA ZA UTOTONI

Wajanja wengi na watu wenye tamaa wanatumia, visingizio vya imani, na tamaduni, kuwarubuni mabinti, na kuwafanya kabisa wapoteze ndoto zao za maisha ya usoni, na kuwafanya wajikute katika ndoa za utotoni, lakini kwa kizazi hiki, jamii iko makini sana, kijana umeumbuka baada ya kujikuta ameshughulikiwa na mzazi wa binti alietaka kurubuni, hebu itazame hii na utoe maoni yako.

MADAWA HOSIPITALINI

mara nyingi watu wakienda hospitalini wanaambiwa kwamba hakuna madawa , lakini wanaelekezwa kwenye maduka fulani , nini ambacho kiko nyuma ya pazia ? tazama hapa ?

ITIKADI TOFAUTI


Changamoto zinazotokana na wanandoa kuwa katika vyama tofauti, umewahi kushuhudia changamoto za namna hii ?, toa maoni yako sasa.

AFYA KUZOROTA

Vifo vya akina mama wajaa wazito vingi vinasababishwa na ukosefu wa huduma  za afya pamoja na wahudumu wa afya kutokuajibika

KAULI ZA VIJANA

Vijana wengi wanashabikia mabadiliko lakini hawajiandikishi na kuchukua vitambulisho vya kupiga kura , sasa mabadiliko wanayoyatarajia, na viongozi waadilifu watapatikana vipi ? Hebu toa maoni yako kuhusiana na jambo hili.

Thursday, November 27, 2014

MTAZAMO POTOFU

Katika jamii mbalimbali kuna watu ambao bado wanabeza wagombea Wanawake, tazama video hii na utoe maoni yako

KATA NGUMI JIIWE

Bwana Mchumiatumbo aliwatumia vijana katika kampeni yake ya kugombea udiwani wa Kata ya Ngumijiwe,aliwapa ahadi lukuki lakini alipopata udiwani akawadharau, sasa hasira ziliwapelekea kufanya mamuzi mabaya ya kumtendea unyama,tazama video hii na utoe maoni yako.

Wednesday, October 8, 2014

Wednesday, October 1, 2014

Monday, June 30, 2014

Monday, March 31, 2014

KUFA KWA NDOTO

Umaskini ni chanzo cha kufa kwa ndoto nyingi hasa pale baba anakuwa ajui umuhimu wa elimu fuatilia simulizi hii...

MKANDA

Kutokuelewana kwa wazazi kunaweza kuwa chanzo cha maendeleo mabaya ya watoto  katika masomo yao na hata maisha yao kwa ujumla fuatilia kisa hiki...

WIZI WA PIKIPIKI

**New

UGOMVI WA MAJIRANI

Maji yamekuwa ni tatizo linalosumbua maeneo mengi nchini, fuatilia simulizi hii kutoka manyara..

ADHA YA MAJI

Maji! maji!....maji ni uhai,lakini tusipo angalia maji yanaweza kuzua matatizo katika jamii,angalia jinsi shida ya maji ilivyo sababisha ugomvi.

FUNDI JOHN

Ng`ombe wa maskini kweli azai fuatilia...

Tuesday, March 11, 2014

BABA MWENYE NYUMBA

Nyumba za kupanga zinasaidia lakini zina matatizo, hasa pale unapokuta baba mwenye nyumba asiye kuwa na maadili. Fuatilia kisa hiki...

TRANSFOMER

Daladala hazikosi vituko, angalia kisa hiki...

BABU MASTER

Imani za kishirikina chanzo cha matatizo katika jamii,tazama kisa hiki, jinsi babu alivyo sababisha majanga...

UZEMBE

Uzembe wa mama wasababisha mtoto kupoteza maisha kwa sumu ya panya,fuatilia kisa hiki chenye mafundisho...

KICHWA CHA FAMILIA

Kijana anafukuza mama yake pamoja na wodogo zake kufuatia ushauri wa mke wake, fuatilia..

NDAKA

Msimamo katika mila na desturi zinachangia katika maambukizi ya VVU.Mila ya utakaso mkoani lindi maarufu kama Ndaka ambayo hufanyiwa mwanamke baada ya kujifungua mtoto aliye fariki inalete kutokuelewana katika familia ya Mzee Lule fuatilia simulizi hii.....

SIMU

Uaminifu katika ndoa,umekuwa ni jambo gumu hasa baada ya kurahisishwa kwa mawasiliano...angalia jinsi simu inavyoweza kuvunja ndoa...

MAISHA

Kuachwa ni shughuli pevu....angalia jinsi bwana Mussa alivyo achwa na mkewe baada ya pombe kumnogea!

BODA BODA

Wahenga walisema ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni...fuatilia kisa cha mwizi aliyegoma kuachiliwa huru ili kuokoa maisha yake....

WEZI

kimbembe huzuka pale vibaka wanapo mpora ngudu wa kibaka mwenzao!fuatilia

YATIMA

Maadili katika jamii yetu yanasikisha hasa pale baba anapo amua kula kuku na mayai yake na kusababisha vilio vilivyo changanyika na mashangao katika familia yake!!!fuatilia simulizi hii..

KAMATA MWIZI

Mshao unampata  mwizi,pale anapoanza kufukuzwa kimyakimya...

BAHATI

Kijana wa kike mwenye ndoto za kufanikiwa kimasomo,anafauru mitihani yake vizuri ili kuendelea mbele lakini kama wasemavyo wahenga penye miti hapana wajenzi ...fuatilia simulizi hii


Thursday, February 13, 2014

TAMAA MBAYA

Vijana wa kike kuozeshwa katika unri mdogo uku wakiachishwa masomo yao na kinyume cha matakwa yao ni changamoto inayo zikumba jamii nyingi mkoani Manyara             simulizi hii inaelezea kisa cha baba aliyeahidiwa ng'ombe nane ili kumuozesha bintiye mwenye umri wa miaka 16.

FIKIRI KABLA YA KUTENDA

Simu inaweza  kutumika kuleta maendeleo, kuleta furaha, kuanzisha mahusiano mazuri, kupata taarifa nzuri na mambo mengine ambayo ni muhimu kwenye maisha yetu ya kila sik. lakini simu ikitumiwa vibaya huweza kuleta majanga........
Simulizi hii ni kuhusu baba aliyemuua mtoto wake mwenyewe kwa sababu ya
 "WRONG NUMBER"

Thursday, February 6, 2014

UVIVU MBAYA

 Vijana tujitume na tufanye kazi kwa bidii,angalia hasara ya uvivu iliyomkuta kijana na familia yake.

MKULIMA HOI

 Pamoja na vijana kujitahidi kufanya kazi za ukulima ili waweze kujikwamua kimaendeleo,ni dhahiri kuwa jitihada hizo zinaweza kuwa mithiri ya mbio za sakafuni ziishiazo ukingoni,endapo akutakuwa na juhudi madhubuti za kuanza kutumia dhana za kisasa kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Saturday, January 18, 2014

Bwana Kazimoto

Filamu hii ni matokeo ya mafunzo ya wakufunzi wa mradi wa Simulizi za vijana yaliyotolewa na TACCI, imefanikishwa kupitia mradi wa TMF kwa kuwawezesha vijana kutoa simulizi kidigitali