Wajanja wengi na watu wenye tamaa wanatumia, visingizio vya imani, na tamaduni, kuwarubuni mabinti, na kuwafanya kabisa wapoteze ndoto zao za maisha ya usoni, na kuwafanya wajikute katika ndoa za utotoni, lakini kwa kizazi hiki, jamii iko makini sana, kijana umeumbuka baada ya kujikuta ameshughulikiwa na mzazi wa binti alietaka kurubuni, hebu itazame hii na utoe maoni yako.
Tuesday, December 9, 2014
MADAWA HOSIPITALINI
mara nyingi watu wakienda hospitalini wanaambiwa kwamba hakuna madawa , lakini wanaelekezwa kwenye maduka fulani , nini ambacho kiko nyuma ya pazia ? tazama hapa ?
ITIKADI TOFAUTI
Changamoto zinazotokana na wanandoa kuwa katika vyama tofauti, umewahi kushuhudia changamoto za namna hii ?, toa maoni yako sasa.
AFYA KUZOROTA
Vifo vya akina mama wajaa wazito vingi vinasababishwa na ukosefu wa huduma za afya pamoja na wahudumu wa afya kutokuajibika
KAULI ZA VIJANA
Vijana wengi wanashabikia mabadiliko lakini hawajiandikishi na kuchukua vitambulisho vya kupiga kura , sasa mabadiliko wanayoyatarajia, na viongozi waadilifu watapatikana vipi ? Hebu toa maoni yako kuhusiana na jambo hili.
Thursday, November 27, 2014
MTAZAMO POTOFU
Katika jamii mbalimbali kuna watu ambao bado wanabeza wagombea Wanawake, tazama video hii na utoe maoni yako
KATA NGUMI JIIWE
Bwana Mchumiatumbo aliwatumia vijana katika kampeni yake ya kugombea udiwani wa Kata ya Ngumijiwe,aliwapa ahadi lukuki lakini alipopata udiwani akawadharau, sasa hasira ziliwapelekea kufanya mamuzi mabaya ya kumtendea unyama,tazama video hii na utoe maoni yako.
Subscribe to:
Posts (Atom)





